Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 18:03

Baraza la usalama la UN bado limegawanyika kuhusu Pyongyang


Kim Song, balozi wa Korea kaskazini katika Umoja wa Mataifa.
Kim Song, balozi wa Korea kaskazini katika Umoja wa Mataifa.

Balozi wa Korea Kaskazini ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa nchi yake itashikilia kwa uthabiti silaha zake za nyuklia

Wakati mzozo wa nyuklia kati ya Marekani na Korea Kaskazini ukiendelea bila ya kuwepo kwa maelewano ya kidiplomasia, baadhi ya wataalamu mjini Washington wanasema kampeni ya taarifa inalenga kuishinikiza Korea Kaskazini inapaswa kuchukuliwa kama mkakati mbadala, huku wengine wakitahadharisha dhidi ya mwelekeo kama huo.

Majadiliano yamekuja wakati Korea Kaskazini ikizidisha mivutano huku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likiwa bado limegawanyika kuhusu namna ya kujibu vitisho vinavyoongezeka vya Pyongyang.

Kim Song, balozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa aliliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu kuwa nchi yake itashikilia kwa uthabiti silaha zake za nyuklia, akisema kamwe hatutafikia muafaka, bila kujali nani atachaguliwa kuwa rais ajaye wa Marekani mwezi Novemba.

Forum

XS
SM
MD
LG