Kishida alishinda kuchukua uwongozi wa chama tawala cha Liberal Demockratik siku ya Jumatano na kumweka katika nafasi ya kua waziri mkuu mpya, akikabiliwa na jukumu kubwa la kushughulikia uchumi uloathirika sana na janga na COVID-19 na kuhakikisha ushirikiano thabiti na Washingtopn.
Kishida amanachukua nafasi ya waziri mkuu Yoshihide Suga anaeacha madaraka mwaka mmoja tu tangu alipoingia madarakani Septemba mwaka 2021.
Akizungumza mara tu baada ya ushindi wake, Kashida ameahidi kuleta mabadiliko na kurudisha sifa za chama baada ya kuzorota kutokana na waziri mkuu Sugu kuwakasirisha Wajapani kwa namna alivyoshughulikia janga la COVID na kushikilia kufanyika michezo ya Olympik ya Tokyo mwaka huu.
“ Mimi Fumio Kishida, nina ujuzi maalumu wa kusikiliza watu. Nimejizatiti kufanya juhudi za kuwa na chama kilicho wazi cha Liberal Democratic na siku za usoni bora kwa japan kwa pamoja na nyie wote. Ninaomba uungwaji mkono wenu wote na msaada hicho ndio pekee kutoka kwangu. Ninatazamia kufanyakazi pamoja na nyie wote na asante.”