Maseneta Warepublican walipiga kura kupinga mswada huo Jumatatu jioni, na kuwalazimisha Wademokrat kuanza kutafuta mbinu mbadala za kuhakikisha kwamba serikali itaendelea na shughuli zake baada ya Alhamisi wiki hii, na kuongeza viwango vya deni, kabla ya wakati ambapo inatarajiwa kushindwa kulipa madeni yake, mwishoni mwa mwezi Oktoba au mwanzoni mwa mwezi Novemba kufika
Maseneta 48 waliunga mkono mswada huo huku 50 wakipinga.
Angalau maseneta 60 wanahitajika kupitisha miswada mingi, kwa mujibu wa kanuni za baraza hilo.
Warepublican wamesema wanataka Wademokrat waongeze viwango vya deni peke yao kwa sababu wanaupinga mpango wao wa matumizi ya trilioni za dola.