Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:04

AMISOM yamuua kiongozi wa al-Shabaab Somalia


Makamanda wa Kikosi cha jeshi la Kenya kwenye operesheni ya AMISOM nchini Somalia
Makamanda wa Kikosi cha jeshi la Kenya kwenye operesheni ya AMISOM nchini Somalia

Wizara ya Ulinzi nchini Kenya imesema kuwa imefanikiwa kumuua Jumamosi, kiongozi wa kikundi cha wapiganaji wa al-Shabaab, Bashe Nure Hassan, baada ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa (AMISOM) kulizima shambulizi la al-Shabaab.

Hassan ambaye ni mkazi wa Kuday, eneo ambako AMISOM na vikosi vya Jeshi la Kenya (KDF) yanalinda amani, alizaliwa na kukua hapo kabla ya kujiunga na kikundi cha kigaidi miaka kadhaa nyuma.

Kwa mujibu wa maelezo ya Kanali Joseph Owuoth vikosi vya AMISOM na vya Kenya vitaendelea kuimarisha ulinzi na kupambana na magaidi kuhakikisha usalama na amani wa taifa la Kenya, na kuendelea kusaidia operesheni za jeshi ya kulinda amani la Umoja wa Afrika (AMISOM) ili kuleta utulivu Somalia.

Kwa mujibu wa taarifa iliotolea Jumamosi na KDF katika mida ya saa tisa mchana magaidi wa al-shabaab walishambulia vikosi vya jeshi la Somalia (SNA) vilivyopo karibu na kambi ya Amisom/KDF katika eneo la Kuday.

Katika jaribio hilo la magaidi wa al-Shabaab wawili kati ya wapiganaji wao walidhibitiwa na wengine wengi wanaoshukiwa kuwa ni wafuasi wa kikundi hicho kujeruhiwa.

Taarifa hiyo imesema kuwa silaha tatu aina ya AK 47, magazine 11 za bunduki hizo, simu ya satellite na risasi 290 pia zilikamatwa.

Hata hivyo taarifa hiyo imeripoti kuwa hakuna yoyote aliyekuwa amejeruhiwa kutoka katika majeshi ya AMISOM/KDF na SNA.

XS
SM
MD
LG