Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 01, 2025 Local time: 06:22

Kinga ya sindano dhidi ya virusi vya Ukimwi yaidhinishwa Marekani


Mtaalamu wa maabara akipima sampuli za damu kuangalia maambukizi ya HIV katika Taasisi ya Afya ya Uzazi na HIV, Johannesburg, Nov. 26 2020.(AP Photo/Denis Farrell)
Mtaalamu wa maabara akipima sampuli za damu kuangalia maambukizi ya HIV katika Taasisi ya Afya ya Uzazi na HIV, Johannesburg, Nov. 26 2020.(AP Photo/Denis Farrell)

Mamlaka ya kudhibiti ubora wa chakula na dawa nchini Marekani imeidhinisha matumizi ya dawa kwa njia ya sindano, kwa watu ambao huenda wakaambukizwa virusi vya Ukimwi baada ya kujikuta katika mazingira hatarishi ya maambukizi.

Dawa hiyo Apretude, itatumika kwa vijana wanaobalehe na watu wazima.

Ni ya kwanza kutolewa kwa njia ya sindano na mtu atadungwa mara tofauti kwa muda wa miezi miwili, na anayepatiwa dawa hiyo anastahili kuwa hajaambukizwa virusi vya Ukimwi na ana uzito wa angalau kilo 35.

Kabla ya dawa hii kuidhinishwa, watu ambao walikuwa wamejikuta katika mazingira hatari ya kuambukizwa virusi vya Ukimwi walikuwa wakimeza vidonge kila siku.

Muungano unaotetea utafiti wa chanjo dhidi ya Ukimwi umesema kwamba utashirikiana na mashirika mengine kuunga mkono hatua hiyo katika sehemu nyingine duniani.

XS
SM
MD
LG