Wakati huo huo msako mkali unaendelea kaika kaunti ya Kirinyaga ambako hukumu hiyo ilitolewa ili kuwadhibiti wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo ya ombaomba.
Hata hivyo wote waliopatikana na makossa hawakupata fedha hizo na watatumikia kifungo hicho huku mikakati ya kuomba warejeshwe kwao ikiandaliwa baada ya kumaliza kifungo.
Aidha, mmoja wao hakujibu mashtaka kwa kuwa ilitambulika kuwa ni bubu. Hakimu ametoa maelekezo kwa mkuu wa mashtaka amtafutie mkalimani kesi yake itakaposikizwa Oktoba 3.
Vyanzo vya habari hizi vimesema kuwa walemavu hao watano wakiwa wanawake na mwanamume mmoja walishtakiwa kwa kuwa nchini Kenya kinyume cha sheria na kusababisha kero kubwa kwa raia.
Wote watano walikiri kuwa waliingia nchini humo kutoka Tanzania na hawakuwa na nyaraka zozote za uraia wa Kenya.
Mshirikishi wa masuala ya kiusalama katika eneo la Kati,Kenya, Anne Ng’etich amesema tayari walemavu wengine 150 wengi wao wana ulemavu unaosababishwa na ukosefu wa chanjo muhimu utotoni wamenaswa.
Alisema baada ya uchunguzi kukamilika baadhi yao watafikishwa mahakamani huku wengine wakirudishwa makwao.
Pia ametoa onya kwa raia wengine wanaojihusisha na vitendo vya namna hii waachane mara moja kwani Serikali (Kenya) iko macho,
Walemavu hao ‘wanawaajiri’ watoto wa maeneo hayo kuzurura pamoja nao huku wakiombaomba fedha kutoka kwa raia na kisha kuwalipa jioni jambo ambalo alisema ni kinyume na sheria za haki za watoto.