Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 21:06

'Serikali itoe majibu ya shambulizi la wanafunzi wa Nairobi University'


Askari wakimkamata mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi.
Askari wakimkamata mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi.

Mbunge wa Embakasi Mashariki nchini Kenya Paul Ongili ambaye ni maarufu kwa jina la Babu Owino amemtaka kaimu Waziri wa Usalama Dr Fred Matiang’i na Inspekta Jenerali wa Polisi, Joseph Boinnet kutoa majibu juu ya kushambuliwa kwa wanafunzi Alhamisi na askari wa kutuliza fujo.

“Tunataka majibu kutoka kwa Waziri na Mratibu wa shughuli za Serikali Matiang’i na Inspekta Jenerali Boinnet juu ya kile kilichojiri katika madarasa na mabweni ya wanafunzi na kuhakikishiwa kwamba maafisa waliohusika na vitendo vya kinyama watachukuliwa hatua mara moja.,” amesema Owino.

Owino pia ameagiza kuwa mara moja Kituo cha polisi cha kati kuwaachia huru wanafunzi waliohusishwa na maadamano ya siku ya Alhamisi.

“Sisi pia tunataka kuachiwa mara moja na bila masharti kaka na dada zetu ambao wameshikiliwa kituo cha polisi,” ameongeza kusema.

Kituo huru cha kumulika vitendo vya polisi (IPOA) kimetangaza Ijumaa kuwa kimeanzisha uchunguzi juu ya madai ya shambulizi yaliyofanywa kwa wanafunzi.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano cha IPOA amesema imetuma kikundi maalum cha dharura kuchunguza mashambulizi hayo wakati wa maandamano yaliyokuwa yanamuunga mkono Babu Owino.

XS
SM
MD
LG