Mmoja wa waliozuiliwa kuhudhuria vikao ni Waziri wa Maji, Ronald Kibuule kwa madai ya kwenda katika ukumbi wa bunge akiwa na silaha.
Wabunge wengine waliosimamishwa kuhudhuria kikao wengi wao ni wa upinzani wanaopinga kufutwa kwa kifungu 102(b) kutoka katika katiba ambayo inakataza watu ambao wanaumri zaidi ya miaka 75 kugombea nafasi ya urais, ambao wamekataa kutoka katika ukumbi wa bunge na kumlazimisha spika kuahirisha kikao.
Wale waliozuiwa kuhudhuria vikao vya bunge ni : Robert Kyagulanyi aka Bobi Wine (Kyaddondo Mashariki), MP Allan Ssewanyana (Makindye Magharibi),Monica Amoding (Wilaya ya Kumi ), Dr Sam Lyomoki (Wafanyakazi) Betty Nambooze (Manispaa ya Mukono) Ibrahim Kasozi (Makindye Mashariki) andMoses Kasibante (Rubaga Magharibi).
Baada ya mgogoro huo, maafisa wa ulinzi wakiwa katika vazi la suti walivamia Ukumbi huo na kuwalazimisha Kyagulanya na Ssewanyana kutoka nje.
Serikali ya Uganda inataka kuondoa ukomo wa umri kwa wagombea urais kitu kilicholeta vurugu Jumatano katika bunge la Uganda.
Hhatua hivyo ya serikali itamwezesha Yoweri Museveni kuendelea na nafasi yake ya urais.
Sheria hizo zilikuwa tayari zimebadilishwa 2005 zikiondoa ukomo wa awamu mbili ambapo ilimwezesha Museveni ambaye sasa ana umri wa miaka 72 na awamu yake ya tano, kuendelea kuwepo katika madaraka.
Chini ya katiba iliyokuwepo Rais Museveni atakuwa amepitiliza umri unaoruhusiwa na katiba kugombea katika uchaguzi wa mwaka 2021.