Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 06:53

WHO, Kenya zazindua ujenzi wa kituo cha kikanda cha dharura za afya


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na wawakilishi wa WHO na wadau wengine, wakati wa uzinduzi wa mpango wa ujenzi wa kituo cha dharura za kiafya mjini Nairobi, Kenya. Julai 9, 2022.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na wawakilishi wa WHO na wadau wengine, wakati wa uzinduzi wa mpango wa ujenzi wa kituo cha dharura za kiafya mjini Nairobi, Kenya. Julai 9, 2022.

Shirika la Afya Duniani, WHO, kwa ushirikaiano na serikali ya Kenya, limezindua mpango wa ujenzi wa kituo cha kikanda cha dharura za matibabu, ambacho ni cha kwanza, katika mpango wa kuanzisha vituo kadhaa barani Afrika.

Akizungumza kwenye hafla iliyofanyika mjini Nairobi, mkurugenzi wa WHO, anayesimamia ukanda wa Africa, Matshidiso Moeti, alisema Kenya itakuwa kitovu cha kikanda cha vifaa vya matibabu, na itasaidia nchi jirani kupata dawa na vifaa vinavyohitajika kwa haraka zaidi kuliko ilivyo sasa.

WHO inasema vituo kama hivyo vitaharakisha mchakato wa majibu ya dharura za kimatibabu katika ukanda huo.

Katibu Mkuu wa WHO Adhanom Gebreyesus aliipongeza serikali ya Kenya, ikiwakilishwa na Rais Uhuru Kenyatta, ambaye aliongoza hafla hiyo, kwa ushirikiano iliyoutoa katika kufanikisha azma hiyo.

Kenyatta alisema kituo hicho kitajengwa katika eneo la ekari 30, karibu na chuo kikuu cha Kenyatta, ambazo zilitolewa na serikali.

Hata hivyo, hakukuwa na ratiba ya wakati kituo hicho kitaanza kufanya kazi kikamilifu.

WHO itaanza kazi ya kusaidia nchi mbalimbali kutoa mafunzo kwa wahudumu wa dharura wa kitaifa mara moja, Moeti alisema, na kuongeza kwamba shirika hilo lina mipango ya kujenga vituo kama hivyo, katika kila nchi barani Afrika.

"Tunaona bara hilo likielezea kwa vitendo azma yake ya kujiandaa vyema kwa janga lijalo ... huu utakuwa mchango wetu katika kusaidia nchi kujenga uwezo wao wa kujiandaa vyema na kuweza kukabiliana vilivyo," Moeti aliliambia shirika la habari la Reuters.

Kwa sasa, shirika la afya duniani linafuatilia matukio ikiwa ni pamoja na uwezekano wa visa vya virusi vya Marburg vinavyoambukiza sana nchini Ghana, surua katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kipindupindu nchini Cameroon - pamoja na COVID-19 katika bara zima.

Mafuriko, ukame, na migogoro, ambayo inaongezeka katika sehemu kubwa ya eneo hilo, pia huathiri afya ya umma.

XS
SM
MD
LG