Kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliitisha maandamano kupinga ongezeko la kodi lililowekwa katika kipindi ambacho watu wengi wanataabika na bei kubwa za bidhaa za msingi kama vile unga wa mahindi.
Mahakama Kuu ya Kenya, iliamuru kwamba ongezeko la kodi liahirishwe lakini serikali imeongeza bei ya mafuta ambayo imepelekea changamoto nyingine za mahakama.
Polisi waliwakamata wafuasi kadhaa wa upinzani katika mji mkuu na magharibi mwa Kenya, ofisi ya shirika la kutetea haki za binadamu nchini kenya- Amnesty international imesema katika taarifa yake , bila kutoa maelezo zaidi.
Hakuna maoni ya haraka kutoka polisi kuhusiana na taarifa hiyo.
serikali imesema ongezeko la kodi , linatarajia kuongeza shilingi bilioni 200 ambazo ni sawa na dola bilioni 1.4 kwa mwaka , ambazo zinahitajika kukabiliana na deni kubwa linaloongezeka na kufadhili miradi ya kufungua nafasi za ajira.
Akihutubia takriban wafuasi 2, 000 Odinga aliishutumu serikali ya rais William Ruto kushindwa kupambana na ughali wa maisha, kuwahadaa wabunge wa upinzani na kubadilisha mfumo wa tume ya uchaguzi.
Forum