Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 05:52

Kenya kuondoa Visa kwa raia wa Comoros


Rais Ruto wa Kenya akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya Nairobi, Mei 5, 2023. Picha na REUTERS/Moniah Mwangi
Rais Ruto wa Kenya akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya Nairobi, Mei 5, 2023. Picha na REUTERS/Moniah Mwangi

Rais wa Kenya William Ruto amesema kwamba anaendelea kupiga hatua katika kuondoa masharti ya utoaji wa Visa kati ya Kenya na Comoros, kabla ya mwaka huu kumalizika.

Akizungumza Alhamisi July 6, wakati wa maadhimisho ya miaka 48 ya uhuru wa Comoros, Ruto amesisitiza kwamba nchi hizo mbili zina ushirikiano wa kihistoria wa kitamaduni na biashara.

Kwa sababu hiyo, amesema kwamba nchi hizo mbili zina uhusiano mzuri wa kidiplomasia na ushirikiano katika sekta mbali mbali.

Ruto amesema kwamba Kenya ipo tayari kueneza ushirikiano na Comoros katika maswala ya elimu, Kilimo, afya na usalama, kwa lengo la kuimarisha Maisha ya raia wa nchi hizo mbili na kujenga ushirikiano mwema katika siku zijazo.

Forum

XS
SM
MD
LG