Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 22:48

Kenya huenda ikakumbwa na mfumuko wa bei wa ndani



Ujenzi wa reli ya Standard Gauge (SGR) katika Mbuga ya Kitaifa ya Nairobi, Kenya, Novemba 21, 2018. Picha na Yasuyoshi CHIBA / AFP.
Ujenzi wa reli ya Standard Gauge (SGR) katika Mbuga ya Kitaifa ya Nairobi, Kenya, Novemba 21, 2018. Picha na Yasuyoshi CHIBA / AFP.

Kenya huenda ikaingia kwenye changamoto mpya ya mfumuko wa bei wa ndani unaotokana na kuelemewa na madeni ambayo hayana uwiano mzuri kati ya matumizi, uwezo wa ulipaji na uzalishaji katika nchi.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Jumatatu, aliyekuwa meneja wa Benki ya Dunia anayeshugulikia mahusiano ya nje kwa nchi za Afrika na pia mkuu wa zamani wa kitengo cha mahusiano na mawasiliano katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) Eric Chinje amesema Kenya lazima izingatie uwiano huo kwa kuwa wakati wote serikali inahitaji mikopo kwa ajili ya uwekezaji.

Chenje alisema mfumuko wa bei hutokea pale nchi inapoelemewa na madeni.

Alisema ukopaji uliokithiri Kenya ulianza wakati wa utawala wa raisi Uhuru Kenyatta ambaye alitaka kudumisha kasi ya ukuaji wa uchumi ilioachwa na utawala wa rais Mwai Kibaki ambaye alimaliza muda wake mwaka 2013.

Kudumisha maendeleo hayo “Kenya ilianza kukopa na kuifanya nchi ianze kutetereka hususani wakati China nayo ilipofungua benki zake tayari kukopesha”aliongeza.

Hata hivyo Mchambuzi wa maswala ya uchumi wa Kenya Bravious Kahyoza, aliiambia Sauti ya Amerika kwamba Kenya inachukua hatua ya kukabialiana na changamoto za kiuchumi ikiwemo upungufu wake wa fedha za kigeni na mafuta.

Na kuongeza kuwa serikali imesitisha baadhi ya miradi muhimu ikiwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara ya kilometa 231 inayotoka Nairobi kwenda Nakuru mpaka Mau ili kubabiliana na nakisi ya bajeti ya zaidi ya asilimia nane kwa mwaka iliyokuwa ikiielemea nchi hiyo katika kipindi cha miaka miaka sita iliyopita.

XS
SM
MD
LG