Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:25

Nguo za mitumba zaharibu mazingira


Pichani wanawake wakitazama mitumba katika jiji la Nairobi, Kenya, tarehe 8 Aprili 2018. Picha na AP/Sayyid Abdul Azim.
Pichani wanawake wakitazama mitumba katika jiji la Nairobi, Kenya, tarehe 8 Aprili 2018. Picha na AP/Sayyid Abdul Azim.

Kenya inaelezewa inafanya biashara kubwa sana ya nguo za mitumba ambazo inakadiria kuna nguo takriban milioni 900 ambazo huingia nchini humo kila mwaka zikitokea Ulaya na Marekani.

Lakini wachuuzi wanasema nguo nyingi zinaishia kwenye majalala, na ripoti iliyoongozwa na Uholanzi inasema karibu theluthi moja ya bidhaa za plastiki kutoka nje hazijawahi kuoza na hivyo huchangia katika uharibifu wa mazingira.

Katika soko la Gikomba, soko ambalo ni kubwa sana nchini Kenya kwa nguo za mitumba, tunakutana na Mwende Mulwa. Mfanyabiashara wa nguo za mitumba analalamikia kile anachokiita ubora duni wa mitumba inayoagizwa kutoka nje. Anaelezea jinsi biashara ya nguo za mitumba ilivyoshamiri na kuwa ni mhimili wa kipato.

Wafanyabiashara kadhaa ambao wameongea na VOA kwenye soko hilo walikuwa na malalamiko yanayofanana. Madai yao yaliungwa mkono na ripoti ya taasisi ya mazingira ya Uholanzi – Changing Markets Foundation.

Ripoti kulingana na utafiti nchini Kenya, kwa kushirikiana na kundi linaloitwa “Clean Up Kenya,” linasema karibu asilimia 30 ya nguo zilizotumika zinasafirishwa kwenda Kenya kutokea Ulaya na Uingereza na zinatengenezwa na vitambaa kama polyster na nylon – vyote ni aina ya plastic ambavyo si vizuri na vinajulikana kwa kiingereza ni petroleum based plastic.

Betterman Simidi ni muanzilishi wa Clean Up Kenya taasisi inayotetea hifadhi ya mazingira ambayo ilikuwa sehemu ya utafiti, na kuongezea “nguo nyingi za mitamba mbazo zinaletwa humu nchini ni za ubora duni sana na nyingi huwa hazitumiki.”

Kiasi cha nguo milioni 900 zile ambazo zimetumika zinapelekwa nchini Kenya kila mwaka, hasa kutoka Ulaya na Marekani kwa mujibu wa Changing Markets Foundation.

Mamlaka inayosimamia mazingira nchini Kenya, National Environment Management Authority inasema itaiangalia ripoti lakini imeongezea kwamba uchafuzi kutoka kwenye taka za nguo za mitumba zile zinazoagizwa kutoka nje haujarekodiwa na hivyo bado haijulikani.

Mamlaka inasema kuna hatua zimewekwa, ikiwemo sheria za utupaji hizo nguo kudhiti zile ambazo zinaagizwa kutoka nje.

Salome Machua ni naibu mkurugenzi wa mamlaka hiyo ambaye anahusika na uimarishaji wa kanuni anaelezea. “Kenya imetia saini Azimio la Basel na azimio hilo limeweka masharti juu ya umuhimu wa taka. Azimio hili linasema kwamba watu ni vyema waweze kushughulikia taka ndani ya maeneo yao.”

Wanaharakati wa mazingira wanashutumu chapa za nguo kutoka nchi zilizoendelea kutupa nguo za zamani kwenye nchi maskini, na kusababisha matatizo ya mazingira na afya kwa jamii wenyeji.

“Kimsingi nguo zote zinazotengenezwa na chapa hizi, zinaishia kwenye nchi maskini. Na hizi chapa lazima zianzie kulipia mwisho wa matumizi ya nguo hizi,” anasema Simidi.

Kenya inaendeleza sheria ya majukumu ya mzalishaji kwamba wale wazalishaji wa nguo hizo wawajibike kwa mwisho wa matumizi wa bidhaa zao.

Kama sekta ya fasheni inavyozidi kukua, biashara na nguo za mitumba imeipa fasheni fursa ya pili katika ulimwengu wa kusini. Lakini wakosoaji hivi sasa wanasema inakuwa kama vile eneo la uchafu wa nguo kwa ulimwengu wa kaskazini.

XS
SM
MD
LG