Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:36

Kenya yaongezewa kiwango cha kukopa kutoka Benki ya Dunia


Rais wa Kenya William Ruto akiwa Addis Ababa Ethiopia, Februari 19, 2023. Picha na EDUARDO SOTERAS/AFP
Rais wa Kenya William Ruto akiwa Addis Ababa Ethiopia, Februari 19, 2023. Picha na EDUARDO SOTERAS/AFP

Kenya na Benki ya Dunia zimeongeza kiwango cha mkopo ili kusaidia bajeti kwa mwaka huu wa fedha kwa hadi dola billioni moja, waraka uliobandikwa katika tavuti ya benki hiyo umeonyesha.

Awali serikali ya Kenya iliashiria kuwa ilikuwa kwenye mazungumzo juu ya mkopo wa kiasi cha dola milioni 750, lakini kiwango hicho kimekuwa kikiongezeka. Waraka huo umeonyesha.

Si serikali ya Kenya wala Benki ya Dunia wamejibu maombi ya kutoa maoni yao.

Mkopo huo bado unahitaji kuidhinishwa na bodi ya benki. Bodhi hiyo ilitarajiwa kufanya uamuzi kabla ya kumalizika kwa mwaka wa wasasa wa fedha wa Kenya hapo Juni 30.

Kenya ilikuwa na sifa za kupewa aina hiyo ya ufadhili mwaka 2019 na tangu wakati huo imeshawahi kupokea mikopo minne ya aina hiyo , mkopo wa mwisho kupokea ulikuwa mwezi Machi.

Uchumi wa Afrika Mashariki unakabiliwa na changamoto nyingi, ikijumuisha mzigo mkubwa wa madeni, bajeti finyu na sarafu dhaifu.

Chanzo cha habari ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG