Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:26

Kamanda wa Hamas aliyeuwawa Lebanon alikuwa mfanyakazi wetu- UNRWA yasema


Wakimbizi wa Kipalestina wakipokea misaada kutoka kwa shirika la UNRWA kaskazini mwa Gaza. July 23, 2024.
Wakimbizi wa Kipalestina wakipokea misaada kutoka kwa shirika la UNRWA kaskazini mwa Gaza. July 23, 2024.

Shirika la  UN kwa ajili ya wakimbizi wa Palestina, UNRWA, limesema kuwa kamanda wa ngazi ya juu wa Hamas aliyeuwawa nchini Lebanon Jumatatu, alikuwa mmoja wa wafanyakazi wake, lakini hakuwa na jukumu lolote kwa kuwa alisimamishwa kazi kwa muda tangu mwezi Machi.

Uhusiano wa Fatah Sharif na kundi la Hamas huenda ukaongeza matatizo ya UNRWA ambalo tayari lina upungufu wa ufadhili wa dola milioni 80 mwaka huu. Wakosoaji wamerejea kuikosoa idara hiyo wakisema kuwa haikuwa ikifanya vya kutosha kuwaondoa wanachama wa Hamas miongoni mwa wafanyakazi wake.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukiichunguza UNRWA tangu Januari mwaka huu baada ya Israel kudai kuwa wafanyakazi wake 12 walihusika kwenye shambulizi la Oktoba 7 dhidi yake ambako watu 1,200 walikufa huku wengine 250 wakitekwa. Madai hayo yalipelekea nchi zaidi ya darzeni moja kusitisha ufadhili wao kwa UNRWA na kusababisha upungufu wa takriban dola milioni 450 kwa shirika hilo.

Hamas limesema kuwa Sharif aliuwawa pamoja na mke wake, na mtoto mmoja wa kike na wa kiume, kwenye shambulizi la anga katika kambi ya wakimbizi ya Al Buss, moja wapo ya kambi 12 zinazotoa hifadhi kwa wakimbizi wa Palestina, karibu na mji wa kusini wa Tyre.

Forum

XS
SM
MD
LG