Zaidi ya wachimbaji haramu 1000 tayari wametoka katika wiki za hivi karibuni wakati polisi wakiendelea na msako, angalau mwili mmoja wa mtu aliyekufa umeletwa juu ya ardhi . Mamia wanaaminika bado wamekwama chini ya ardhi kwenye shimo lenye kina cha zaidi kilomita 2.
Taasisi za kiraia zinaowawakilisha wale waliobaki katika machimbo ya Stilfontein zimesema wachimbaji hao wako tayari kutoka , lakini operesheni za polisi zinaongeza muda wao wa kuchimba, jambo ambalo katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini
Afrika Kusini, Zwelinzima Vavi ameelezea kuwa ni sawa na kifo cha taratibu.
Msemaji wa SAPS Brigedia Athlenda Mathe alisisitiza nia yao ya dhati ya uokoaji. “mamlaka yetu iko wazi, ni kuzuia na kupambana na uhalifu na bado tunaona kwamba kinachoendelea huko chini ni uhalifu mtupu. Shughuli ya uokoaji inaendelea, alisema Mathe katika mahakama kuu ya Pretoria.
Forum