Takriban maafisa wa usalama 24,000 watapelekwa Hiroshima wakati wa mkutano wengi wakitoka maeneo mengine ya nchi.
Kabla ya mazungumzo ya Mei 19 hadi 21 , polisi wa doria wamekuwa wakipita kati ya vikundi vya watalii katika bustani maarufu ya peace park iliyoko magharibi mwa mji huo.
Wafanyakazi wa usalama pia walikuwa wakipita kwenye eneo la mto ambao unapita kwenye maeneo kama vile Atomic Bomb Dome kwa kutumia helikopta.
Hatua zimechukuliwa nje ya mji ikiwemo ikiwemo mji mkuu wa Tokyo ambako kuna ujumbe wa onyo la kuwepo ulinzi mkali kwa ajili ya mkutano huo.
Miji mikubwa nchini Japan kwa ujumla haina mapipa ya taka katika maeneo ya umma lakini maafisa wa usalama wamekuwa wakifunga maeneo mengine yanayoweza kuwa na tishio.