Waziri huyo amesema hayo wakati wa kufunga mkutano wao wa G7 na kueleza kuwa walikuwa na nia ya dhati kuinua na kuweka vikwazo dhidi ya Moscow.
Wakizungumzia kuhusu China, Hayashi alisema mawaziri wa G-7 walisisitiza umuhimu wa kufanya mazungumzo ya wazi na kuwasilisha wasiwasi wao moja kwa moja.”
Hayashi alisisitiza umuhimu wa kuwa na amani na uthabiti nchini Taiwan na kusema kuwa mawaziri wa mambo ya nje katika mkutano huo wameapa kuendelea na juhudi za kidiplomasia.
Viongozi na mawaziri wa mambo ya nje wa G-7 hasa Ufaransa na Ujerumani hivi karibuni waliitembelea China na kumekuwa na wasiwasi mkubwa unaokua baada ya Beijing hivi karibuni kutuma ndege za kivita na meli kuzingira Taiwan.
Beijing imekuwa ikiongeza kwa kasi silaha za nyuklia na kuchukua msimamo mkali zaidi kwa madai yake katika South China sea na kutengeneza mazingira ya uchokozi.