Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 15:56

Israel yafanya mashambulizi mapya Ukanda wa Gaza


Moshi wasambaa katika eneo la Ukanda wa Gaza kufuatia mashambulizi ya angani na ardhini yanayofanywa na jeshi la Israel dhidi ya wapiganaji wa Hamas.
Moshi wasambaa katika eneo la Ukanda wa Gaza kufuatia mashambulizi ya angani na ardhini yanayofanywa na jeshi la Israel dhidi ya wapiganaji wa Hamas.

Wakati huo huo Marekani inakusanya washirika wake kuzilinda meli ambazo zinapita katika bahari ya sham kutoka kundi la waasi wa kihoudhi linaloungwa mkono na Iran huko Yemen.

Jeshi la Israel limesema Jumanne malengo yake ya karibuni ni pamoja na maeneo yanayotumiwa na Hamas na kwamba wanajeshi wameharibu handaki kusini mwa Gaza.

Wanamgambo wa Hamas wanaodhibiti wizara ya afya ya Gaza, wamesema mashambulizi ya Israel yameuwa takriban watu 20 huko Rafah , mji ulioko kusini karibu na mpaka wa Misri ambako maelfu ya raia wamekimbilia.

Mapigano mapya yanakuja wakati ambapo baraza la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kupiga kura azimio linalotaja kusitishwa mapigano katika ukanda wa Gaza ili kufanikisha ufikishaji misaada ya kibinadamu kwa raia wa palestina wenye shida ya chakula, maji na dawa.

Habari hii inatokana na mashirika mbalimbali ya habari.

Forum

XS
SM
MD
LG