Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 13:36

Iran yarusha satelaiti kwenye anga za juu kwa kutumia roketi


Picha ya maktaba ya roketi ya Iran ikiwa tayari kurusha satelaiti kwenye anga za juu.
Picha ya maktaba ya roketi ya Iran ikiwa tayari kurusha satelaiti kwenye anga za juu.

Iran Jumamosi imerusha satelaiti kwenye anga za juu kwa kutumia roketi iliyotengenezwa na jeshi, kwa mujibu wa ripoti ya chombo cha habari cha serikali.

Hatua hiyo ni ya karibuni zaidi, kwenye programu inayoshukiwa na magharibi kuwa huenda ikasaidia Tehran kuimarisha mpango wake wa silaha. Iran imesifu hatua hiyo kama yenye fanaka ikiwa ya pili ya kurusha satelaiti kwenye anga za juu kwa kutumia roketi.

Video iliyorushwa baadaye na chombo cha habari cha serikali ilionyesha roketi ikirushwa kutoka mahala maalum pa kijeshi pa kurushia roketi, pakiaminika kuwa kitongoji cha mji wa Shahroud, kilomita 350 mashariki mwa mji mkuu, Tehran.

Zoezi hilo limefanyika wakati hali ya taharuki ikitanda kwenye eneo zima la Mashariki ya Kati, kufuatia vita vinavyoendelea kati ya Israel na Hamas kwenye Ukanda wa Gaza, na ambavyo Iran imeshiriki kwa kurusha makombora pamoja na ndege zisizo na rubani dhidi ya Israel.

Wakati huo huo, ripoti zimesema kuwa Iran inaendelea kurutubisha madini yake ya uranium kuelekea viwango vya kutengeneza silaha, na kuzua wasi wasi miongoni mwa wataalam wa usafirishaji wa silaha, kuhusu program ya Tehran.

Forum

XS
SM
MD
LG