Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 15:40

Ukraine yamuita balozi wa Iran juu ya madai ya Iran kuipa makombora Russia


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy

Wizara ya mambo ya nje ya Ukraine Jumatatu ilimwita Balozi mdogo wa Iran Shahriar Amouzegar, kupinga tetesi kwamba Tehran inaipa Russia makombora ya masafa marefu.

Wizara hiyo ilisema kwenye mtandao wa Telegram kwamba imempa Amouzegar onyo kali kwamba uthibitisho wa kutoa makombora hayo kwa Russia utakuwa “na matokeo mabaya na yasiyoweza kurekebishwa” katika uhusiano wa nchi zao mbili.

White House iliiambia VOA wiki liyopita kwamba “imeshtushwa” na ripoti za vyombo vya habiri vya nchi za Magharibi ambazo hazijathibitishwa, kwamba Iran ilituma idadi kubwa ya makombora huko Russia ili yatumiwe dhidi ya Ukraine.

Gazeti la Wall Street Journal liliripoti siku ya Ijumaa kwamba maafisa wa Marekani na Ulaya ambao hawakutajwa majina, walibaini katika siku za hivi karibuni kwamba Iran iliipa Russia makombora ya masafa marefu.

Kremlin ilikanusha ripoti hizo na maafisa wa Iran Jumatatu walikanusha kutoa makombora hayo kwa Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG