Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanaani, amesema taarifa za vyombo vya habari vya kizayuni kwamba sehemu iliyo na washirika wake au inayoshikiliwa na Iran imeshambuliwa.
Shirika la habari linalomilikiwa na serikali ya Iran limesema kwamba Idadi ya watu waliofariki katika shambulizi hilo la usiku wa kuamkia leo, imeongezeka na kufikia watu 14. Zaidi ya watu 40 wamejeruhiwa.
Shirika rasmi la habari la Syria la SANA, limeripoti kwamba makombora ya Israel yamepiga sehemu kadhaa katikati mwa Syria, na kuharibu barabara kuu katika mkoa wa Hama na kusababisha moto.
Mojawapo ya shambulizi limelenga kituo cha utafiti wa kisayansi mjini Maysaf, jingine limepiga sehemu ambako makundi ya wapiganaji yanayoungwa mkono na Iran na wataalam wao huwa wanafanyia shughuli zao za kutengeneza silaha.
Vyombo vya habari vya Syria vile vile vimeripoti mashambulizi katika mji wa Tartous. Jeshi la Israel halijatoa taarifa yoyote.
Iran imefutilia mbali ripoti kwamba imetuma makombora nchini Russia. Hii ni baada ya Marekani kuwaarifu washiirika wake kwamba Iran imetuma makombora ya masafa mafupi nchini Russia, kutumika katika vita vyake nchini Ukraine.
Forum