Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:49

Israel yadai imewauwa wanamgambo wa Kipalestina Ukingo wa Magharibi


Israel imesema Alhamisi imewauwa wanamgambo sita wa Kipalestina katika mapigano mapya ya Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu na walowezi, akiwemo mtoto wa mwanamgambo mashuhuri aliyefungwa gerezani.

Mashambulizi hao ya sasa yalikuwa ni sehemu ya uvamizi mkubwa zaidi katika eneo hilo katika wiki iliyopita ambayo Wapalestina wanahofia kuwa inaweza kuongeza vita vya Israel dhidi ya wanamgambo wa Hamas huko Gaza.

Wizara ya Afya ya Palestina imesema mashambulizi ya usiku katika mji wa Tubas ulioko kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi uliuawa watu watano, akiwemo Mohammed Zubeidi, mtoto wa Zakaria Zubeidi, kamanda maarufu wa wanamgambo wakati wa uasi wa pili wa Wapalestina mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Mzee Zubeidi alishiriki katika kutoroka gerezani mwaka 2021 lakini alikamatwa na kurejeshwa jela siku chache baadaye.

Forum

XS
SM
MD
LG