Al Hassan alikutwa na hatia Juni 26 kwa jukumu lake katika polisi ya Kiislamu wakati waasi walipoikamata Timbuktu. Mashtaka yalijumuisha mateso na vitendo vya ukatili.
Majaji walimkuta na hatia Al Hassan akiwa na mchango mkubwa katika kundi la Kiislamu la Ansar Dine ambalo liliweka sheria ya Sharia katika mji.
Hata hivyo Al Hassan alikanusha mashtaka , mawakili wake walisema kwamba alikuwa anajaribu kurejesha utaratibu wakati wa ghasia.
Jaji Antoine Kesia- Mbe Mindua amesema: βAl Hassan amekutwa na hatia na kutokana na uamuzi wa wengi katika uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, ikiwemo mateso , ukatili, na hasira za ukiukwaji wa utu kwa kuwachapa viboko hadharani watu 13 wa Timbuktu.β
Forum