Utawala wa kijeshi pia ulipiga marufuku kwa muda vyombo vya habari vya ndani kwa kutumia ripoti za vyombo vya habari vya kimataifa, ripoti zimesema.
Baraza kuu la mawasiliano nchini Burkina Faso, au CSC, inaituhumu Sauti ya Amerika kwa kuwavunja moyo wanajeshi nchini Burkina Faso na katika nchi jirani ya Mali katika matangazo yake ya tarehe 19 Septemba, kulingana na ripoti za vyombo vya habari. Mahojiano ya VOA yalipeperushwa baadaye na chombo cha habari cha ndani cha kujitegemea, kulingana na shirika la habari la Reuters.
Katika taarifa ya kupiga marufuku vyombo vya habari vya ndani kwa kutumia ripoti za vyombo vya habari vya kimataifa, CSC imesema ilibaini “usambazaji wa habari zenye nia ovu na za kuegemea” unaofanywa na vyombo vya habari vya ndani ambavyo vinatumia ripoti za vyombo vya habari vya kimataifa.
Katika taarifa hiyo ambayo haikuitaja hasa VOA, CSC ilisema ripoti kama hizo zinaonekana “kufumbia macho kwa siri ugaidi.”
Forum