Issa Kaou N’Djim ambaye awali alimuunga mkono kiongozi wa sasa wa kijeshi wa Mali , Kanali Assimi Goita, alikamatwa kwa tuhuma za kumtusi kiongozi wa taifa jirani, ambayo ni hatia nchini Mali, mfanyakazi mmoja wa mahakama amesema.
Mafanyakazi huyo aliambia shirika la habari la AP bila kutaka kutajwa kuwa hakuwa na idhini ya kuzungumza na wanahabari. N’Djim mwishoni mwa wiki kwenye televisheni ya Joliba alisema kuwa viongozi wa kijeshi wa Burkina Faso, ambao ni washirika wa karibu wa Mali, walidanganya kuhusu jaribio na mapinduzi la Septemba.
Mwanasiasa huyo sasa amezuiliwa kwenye jela kuu mjini Bamako kulingana na Ousmane N’djim, ambaye ni mtoto wake wa kiume. Mkuu wa televisheni ya Joliba pia ameitwa ili kuhojiwa na mamlaka. Mali na Burkina Faso zimetawaliwa kijeshi tangu mapinduzi ya 2020 na 2022 mtawalia, sababu kubwa zikiwa ni kutoridhika na serikali za awali zilizochaguliwa kidemokrasia.
Mali, Burkina Faso na Niger ambayo pia inaongozwa na kundi la kijeshi wameunda muungano wa Alliance of Sahel States, au AES.
Forum