Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:52

Hospitali China zakabiliwa na wimbi jipya la COVID


Hali ya maambukizi mapya yaripotiwa nchini China, huku hospitali zikiwa hazina vitanda vya kutosha.
Hali ya maambukizi mapya yaripotiwa nchini China, huku hospitali zikiwa hazina vitanda vya kutosha.

Hospitali nchini China zinakabiliwa na wimbi jipya la maambuklizo ya COVID.

Moja huko Shanghai imesema inatarajia nusu ya watu milioni 25 katika mji huo `kuambukizwa mwishoni mwa wiki baada ya Krismas.

Huko Beijing wafanyakazi wa huduma za afya wamesema wagonjwa wanaweza kurudishwa kutokana na ukosefu wa vitanda na rasilimali.

Howard Bernstein ni daktari katika hospitali ya United Family mjini humo na anaeleza: “ Hospitali imejaa kuanzia juu hadi chini, kwa hiyo chumba cha dharura, kimejaa watu. Wengi wamelazwa hospitali, hali haionekani kuwa ya nafuu kwa siku moja au mbili.

Watu wanaendelea kufika kwenye chumba cha dharura, lakini hawawezi kwenda juu katika vyumba vya hospitali. Kwa hiyo wamekwama kwenye chumba cha dharura.”

Ongezeko la maambukizo limekuja baada ya serikali ya rais Xi Jinping kufuta ghafla masharti yenye lengo la kuzuiya kuenea kwa virusi.

Rais wa China Xi Jinping
Rais wa China Xi Jinping

Vyombo vya habari vya serikali vimesema wafanyakazi walioko mstari wa mbele wameambiwa wafanye kazi hata wakati ambapo wanaugua na wale waliostaafu wamerejeshwa kazini.

XS
SM
MD
LG