Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:10

Mohammed bin Salman amempokea Xi Jinping huko Riyadh


Mrithi wa kiti cha ufalme wa saudi Arabia, Mohammed Bin Salman akipeana mkono na Rais wa China Xi Jinping mjini Riyadh, Saudi Arabia, Dec. 8, 2022.
Mrithi wa kiti cha ufalme wa saudi Arabia, Mohammed Bin Salman akipeana mkono na Rais wa China Xi Jinping mjini Riyadh, Saudi Arabia, Dec. 8, 2022.

Wajumbe wa kikosi cha walinzi wa kifalme wa Saudi Arabia waliokuwa wamepanda farasi na kubeba bendera za China na Saudi Arabia walilisindikiza gari la Xi wakati likiingia katika kasri la kifalme mjini Riyadh

Mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman amempokea Rais wa China Xi Jinping siku ya Alhamisi wakati kiongozi huyo wa China akitangaza "enzi mpya" katika uhusiano na nchi ya Kiarabu, huku makaribisho ya kifahari yakiashiria nia ya Riyadh ya kuimarisha uhusiano na Beijing licha ya tahadhari ya Marekani.

Wajumbe wa kikosi cha walinzi wa kifalme wa Saudi Arabia waliokuwa wamepanda farasi na kubeba bendera za China na Saudi Arabia walilisindikiza gari la Xi wakati likiingia katika kasri la kifalme mjini Riyadh, ambako Mwanamfalme Mohammed, mkuu wa kampuni kubwa ya mafuta, alimsalimia kwa tabasamu la furaha.

Ilikuwa kinyume kabisa na makaribisho ya hali ya chini aliyopatiwa mwezi Julai kwa Rais wa Marekani Joe Biden ambaye uhusiano wake umevurugwa na sera ya nishati ya Saudi Arabia na mauaji ya Jamal Khashoggi ya 2018 ambayo yalikuwa yamegubika ziara hiyo mbaya.

Marekani ikiangalia kwa makini ukuaji wa China na uhusiano wake na Riyadh ilisema Jumatano kuwa ziara hiyo ni mfano wa majaribio ya China ya kuwa na ushawishi duniani kote na hautabadilisha sera ya Marekani kwa Mashariki ya Kati.

XS
SM
MD
LG