Makundi yote mawili ambayo yamekuwa yakifanya mazungumzo tofauti na wapatanishi wa Misri huko Cairo, wamekataa kuridhia makubaliano yoyote mbali na uwezekano wa kuwaachia mateka zaidi waliotekwa Oktoba 7 wakati vita vilipozuka huko Kusini mwa Israel.
Misri ilitoa “mwelekeo” unaoungwa mkono na wapatanishi wa Qatar, ambao unahusisha sitisho la vita kwa mabadilishano ya kuachiliwa kwa mateka zaidi, na kupanua makubaliano zaidi yatakaohusisha sitisho la kudumu pamoja na kuuondoa utawala huko Gaza ambao kwa sasa inaongozwa na Hamas
Misri ilitoa pendekezo la uchaguzi wakati ikiihakikishia Hamas kuwa wajumbe wake hawatafukuzwa au kushitakiwa, lakini kundi hilo la Kiislamu limekataa makubaliano ya aina yoyote mbali na kuachiliwa kwa mateka, vyanzo vimesema. Zaidi ya mateka 100 wanaaminika bado wanashikiriwa huko Gaza.
Afisa wa Hamas ambaye aliitembelea Cairo hivi karibuni amekataa kutoa tamko la moja kwa moja kuhusiana na mapendekezo yaliyolenga makubaliano ya muda ya kibinadamu na kuonyesha kuwa kundi hilo limekataa kwa kurudia msimamo wake rasmi.
‘Hamas inataka kumaliza uchokozi wa Israel dhidi ya watu wetu, mauaji na mauaji ya kimbari, na tumejadili na ndugu zetu wa Misri jinsi ya kufanya” afisa huyo aliliambia shirika la habari la Reuters.
Forum