Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 15:52

Gavana wa Mombasa aamuru vituo vinavyouza gesi kinyume cha sheria kufungwa


Gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir akikagua eneo lililowekwa mitungi ya gesi mjini Mombasa.
Gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir akikagua eneo lililowekwa mitungi ya gesi mjini Mombasa.

Kufuatia mkasa wa mlipuko wa gesi eneo la Embakasi, mjini Nairobi mwishoni mwa wiki, miji mengine sasa inachukua tahadhari ili kuepusha maafa sawia na hayo siku za usoni.

Mjini Mombasa Gavana wa jimbo hilo Abdulswamad Sharrif Nassir ameamrisha kufungwa kwa maduka na vituo vya uuzaji gesi kinyume na sheria, kama anavyoripotia Amina Chombo.

Washukiwa wa kiwanda cha gesi cha Embakasi, Nairobi kilichosababisha vifo vya watu saba na mamia kujeruhiwa, wakiendelea kuzuiliwa na polisi, serikali ya jimbo la Mombasa , imefunga vituo vya biashara za gesi vinavyoendeshwa kinyume na sheria.

Akifanya ukaguzi wa vituo vya uuzaji na upakiaji wa gasi Gavana wa Mombasa, Abdulswamad Sharrif Nassir, akiambatana na maafisa wa mamlaka husika za kudhibiti uuzaji wa Gas Kenya, amesema kuwa hakuna mfanyibiashara atakaeruhusiwa kuendesha biashara hio bila leseni nne zilizoidhinishwa kisheria.

Leseni hizo ni pamoja na ile ya kutoka kwa mamlka ya mazingira Nema, mamlaka ya kudhibiti kawi na petrol, KEPRA , ile ya ukaguzi kutoka idara ya moto, na leseni ya kuendesha biashara ya serikali.

Aidha ameonya kampuni za usambazaji gesi dhidi ya kuuza gas kwa maduka ambayo hayana vibali badala yake wasamabze gasi hio kwa vituo vya uuzaji mafuta ya petrol.

Hatua ya serikali ya Mombasa inajiri wakati ambapo aliyekua mmiliki wa kiwanda cha gesi Derrick Kimathi , pamoja na joseph Makau, David Walunya Ong’are na Mariam Mtete Kioko ambao ni maafisa wa mamla ya kitaifa ya kusimamia mazingira, Nema, wanaendelea kuzuiliwa na polisi kwa siku 21 kuruhusu uchunguzi kukamilika.

Polisi wanasema wanachunguza Mauaji, njama ya kutenda uhalifu , Vitendo vya Uzembe, kusababisha Madhara na matumizi mabaya ya afisi zao dhidi ya washukiwa.

-Imetayarishwa na mwandishi wa VOA, Amina chombo, Mombasa

Forum

XS
SM
MD
LG