Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 03:13

DRC yawasilisha malalamishi rasmi tena kwa ICC kutaka M23 ichukuliwe hatua


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumanne iliwasilisha malalamishi mengine rasmi, kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), kuitaka kuhakikisha kwamba inaangazia kile inachokiita uporaji wa kimfumo, wa maliasili zake, mashariki mwa nchi hiyo.

DRC inasema uhalifu huo unafanywa na wanajeshi wa Ulinzi wa Rwanda (RDF) na waasi wa kikundi cha waasi cha M23.

ICC tayari imekuwa ikifanya uchunguzi mashariki mwa Kongo tangu 2004 na haijabainika kama malalamishi hayo mapya yatabadilisha mwelekeo wa mahakama hiyo.

"Serikali ya DRC inasalia na wasiwasi mkubwa kuhusu mateso ya wakazi katika sehemu ya eneo lake iliyoathiriwa na vitendo vilivyoelezewa katika kesi hii," Wizara ya Sheria ya Kongo ilisema katika taarifa.

Lengo la hoja hiyo litakuwa kuchunguza na kumfungulia mashtaka mtu yeyote aliyehusika katika ukiukaji wa haki za binadamu kati ya 2022 na 2023, iliongeza.

Kundi la waasi la M23 linaloongozwa na Watutsi lilianzisha mashambulizi mapya mashariki mwa Kongo mwezi Machi mwaka jana, na kuteka miji na vijiji katika eneo linalopakana na Uganda. Mapigano hayo yalipelekea zaidi ya watu milioni 1 kukimbia makwao.

Kongo imeishutumu nchi jirani ya Rwanda kwa kuunga mkono kundi la M23. Serikali ya Rwanda imekanusha shutuma hizo.

Forum

XS
SM
MD
LG