Ziara hiyo inafanyika wakati asilimia kubwa ya sekta ya madini ya DRC ipo chini ya usimamizi wa China.
Tshisekedi anatarajiwa kuisukuma Beijing kufanya mashauriano mapya kwa miktaba ya kiasi cha dola bilioni 6.2 ya madini, iliyosainiwa na kampuni za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 2008 wakati wa utawala wa Rais Joseph Kabila.
DRC pia huenda ikaomba msaada wa China kukabiliana na makundi ya waasi mashariki mwa Congo.
Ziara ya Tshisekedi nchini China ni ya kwanza tangu alipoingia maadarakani mwaka 2019. Inajiri wakati DRC inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu mwezi Desemba mwaka huu.
Kulingana na waziri wa mambo ya nje, ambaye alifanya kikao na naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje wa DRC Christophe Lutundula, China ipo tayari kushirikiana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mradi wa ujenzi wa barabara na reli.
DRC ni mzalishaji mkubwa wa madini ya Cobalt kote duniani, na madini mengine ya almasi, dhahabu, Lithium na mengineyo. China ni mfanyabiashara mkubwa na mshirika wa DRC.
Forum