Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 01, 2025 Local time: 06:46

Dola bilioni 100 zilizotengwa kusaidia athari za Corona zimeibiwa Marekani

Mfano wa dola ya Marekani
Mfano wa dola ya Marekani

Karibu kiasi cha dola bilioni 100 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kusaidia biashara na watu waliopoteza kazi kutokana na janga la virusi vya Corona nchini Marekani zimeibiwa.

Makadirio ya kiasi hicho cha pesa ni kulingana na taarifa za maafisa wa ujasusi na takwimu za wizara ya kazi na usimamizi wa biashara ndogo ndogo. Taarifa hiyo ni kulingana na Roy Dotson msimamizi wa idara ya kitaifa ya kurejesha mali zilizopotea kwa njia ya ulaghai wakati wa majanga.

Maafisa hawakujumuisha kesi za ulaghai kuhusiana na janga la corona ambazo tayari zimefikishwa mahakamani na wizara ya haki. Kesi nyingi zinatokana na ulaghai wa watu kudai mafao kwa vile hawana ajira.

Jengo la wizara ya kazi Marekani
Jengo la wizara ya kazi Marekani

Wizara ya kazi imeripoti kwamba karibu dola bilioni 87 huenda zililipwa kimakosa kwa watu waliodai kwamba hawakuwa na ajira idadi kubwa ya madai hayo yakiwa ya ulaghai. Maafisa wa ujasusi walisema kwamba wamekamata kiasi cha dola bilioni 1.2.

Uchunguzi unaendelea kuhusu pesa zilizotolewa kwa watu waliodai kutokuwa na ajira sawa na ulaghai kupitia kwa mikopo.

XS
SM
MD
LG