Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:47

Cuba yapata rais mpya


Rais wa zamani Raul Castro akiwa na Mrithi wake Rais Miguel Diaz-Canal (kulia), Havana, Cuba, Aprili 18, 2018.
Rais wa zamani Raul Castro akiwa na Mrithi wake Rais Miguel Diaz-Canal (kulia), Havana, Cuba, Aprili 18, 2018.

Miguel Diaz-Canel ametangazwa Alhamisi kuwa rais mpya wa Cuba, ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 60 cha utawala wa kikomunisti kupata rais nje ya familia ya Castro.

Diaz-Canel mwenye umri wa miaka 57, ni mgombea pekee katika nafasi hiyo ya urais, na ameibuka mshindi kuongoza kwa miaka mitano, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya taifa vya nchi hiyo.

Hatua hiyo ilikuwa haijatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika utawala huo. Wakati akiapishwa Alhamisi, Diaz-Canel aliahidi kuendelea na mfumo wa mapinduzi ya kisoshalisti yalioasisiwa na Castro.

“Ridhaa iliyotolewa na wananchi kwa bunge hili ni kuwezesha mapinduzi ya Cuba kuendelea katika wakati huu muhimu wa kihistoria,” Diaz-Canel amesema.

Diaz-Canel, makamu wa rais wa zamani, ni kutoka mrengo wa kisoshalisti anaependelea mabadiliko na anakubalika na watangulizi wake wanaostaafu waliopingania mapinduzi ya nchi hiyo.

Anamrithi Raul Castro mwenye umri wa miaka 86, ambaye ameachia madaraka baada ya kutumikia wadhifa wa urais kwa miaka 10. Kaka yake Raul Castro, Fidel, alitumikia nafasi ya uwaziri mkuu na urais baada ya mapinduzi ya mwaka 1959 mpaka alipokuwa mgonjwa mwaka 2006.

Wakati kupokezana madaraka huko kunawapa fursa viongozi vijana, Raul Castro na viongozi wokongwe wengine wanamapinduzi, wanatarajiwa kuendelea kushikilia madaraka katika Chama cha Kikomunisti. Castro atabakia kuwa kiongozi wa chama.

XS
SM
MD
LG