Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:19

Acacia yapoteza pato la asilimia 50 Tanzania


Machimbo ya Barrick Gold
Machimbo ya Barrick Gold

Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia imeripoti Alhamisi kuwa imepoteza pato lake kwa asilimia 50 katika awamu ya kwanza baada ya kupunguza operesheni zake za uchimbaji katika machimbo yake maarufu nchini Tanzania kufuatia mgogoro wa kodi baina yake na serikali ya nchi hiyo.

Acacia, ambayo ni kampuni moja wapo inayoendeshwa na kampuni mama ya Canada Barrick Gold na ikiwa ndiyo kampuni kubwa ya uchimbaji Tanzania, imesema uzalishaji wa dhahabu ulishuka kwa asilimia 45 katika kipindi cha kwanza kabla ya mwaka mmoja kufikia uzani wa aunsi 120,981, ikisababishwa hasa na uzalishaji mdogo katika mgodi mkuu wa kampuni hiyo ulioko eneo la Bulyanhulu.

Hisa za kampuni ya Acacia zilizo orodheshwa katika soko la hisa Uingereza ziliporomoka kwa asilimia 8.8 na sasa zimeshuka kwa zaidi ya asilimia 70 tangia Tanzania ilipoanzisha katazo la kusafirisha malighafi inayotokana na machimbo ya dhahabu mwezi Machi 2017.

Kampuni hiyo iliweza kufikia malengo yake yam waka, ikiwa imekusudia kuzalisha kati ya aunsi 435,000-475,000, au angalau asilimia 38 chini ya kiwango kilichozalishwa mwaka 2017, kwa gharama ya dola 935-985 kwa aunsi.

Mapema mwaka 2017 serikali ya Tanzania ilianza kutilia mashaka utendaji wa makampuni ya kuchimba madini nchini humo hasa baada ya kuaminika kuwa kiasi kisichojulikana cha mchanga wenye madini kinatolewa nje ya nchi bila udhibiti mzuri.

Serikali ya Rais John Pombe Magufuli iliunda tume ya uchunguzi kufuatilia suala hilo na mwezi uliopita matokea ya uchunguzi huo yalionyesha kuwa Tanzania imekoseshwa trillion za mapato kutokana na mauzo ya madini ya mchanga unaotolewa nje na makampuni hayo.

Moja ya kampuni kubwa iliyomulikwa katika mgogoro huo ilikuwa Acacia ambayo kampuni yake mama ni Barrick Gold Corporation yenye makao yake makuu nchini Canada. Barrick Gold ni moja ya kampuni kubwa sana za uchimbaji madini duniani ikiwa inaendesha uchimbaji katika mabara yote ya dunia.

XS
SM
MD
LG