Bendera zimepepea nusu mlingoti mjini Beijing leo alhamisi.
Li, aliyebobea katika maswala ya uchumi na mzungumzaji mzuri wa kiingereza, alifariki dunia wiki iliyopita mjini Shanghai, akiwa na umri wa miaka 68.
Kifo chake kimetokea miezi michache baada ya kujiuzulu kutoka nafasi ya pili ya uongozi wa China.
Li amekuwa mtetezi wa ukombozi wa kisiasa na mabadiliko ya kiuchumi lakini alikuwa ametengwa katika mfumo wa utawala wa Rais wa China Xi Jinping aliyekuwa na madaraka ya kusimamia karibu kila kitu.
Chama cha kikomunisti kinachotawala nchini China, kimesema katika taarifa rasmi ya kuomboleza kwamba Li alikuwa kiongozi aliyebobea na mwaminifu kwa chama.
Forum