Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 20:48

Bunge la Marekani lapitisha sheria inayoondoa ukomo wa deni la serikali

Picha kutoka katika Televisheni ya Baraza la Seneti ikionyesha matokeo ya kura ya kupitishwa kwa mswaada wa kuondoa ukomo wa deni la serikali kwa kura za ndiyo 63 na siyo 36, kuanzia Juni 1, 2023, iliyofanyika katika Baraza la Seneti, Bungeni mjini Washington.

Baraza la Seneti la Marekani Alhamisi limepitisha sheria ya pande mbili inayoungwa mkono na Rais Joe Biden ambayo inaondoa ukomo wa deni la serikali la dola Trilioni 31.4 na kuepuka kwa mara kwanza kwa serikali kushindwa kutimiza majukumu yake ya kifedha.

Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Maseneta walipiga kura 63-36 waliidhinisha mswaada uliopitishwa jumatano na baraza la wawakilishi huku wabunge wakiharakisha kushindana na wakati kufuatia miezi kadhaa ya malumbano kati ya Wademocrat na Warepublican.

Wizara ya fedha ilionya kuwa isingeweza kulipa gharama zake ifikapo Juni 5 kama bunge litashindwa kuchukua hatua ifikapo muda huo.

Biden amepongeza hatua iliyochukuliwa kwa muda muafaka na bunge . “ makubaliano haya ya pande mbili ni ushindi mkubwa kwa uchumi wetu na wamarekani,” alisema hayo rais Mdemocrat katika taarifa yake , akiongeza kuwa atatia saini kuwa sheria haraka iwezekanavyo.

Biden alihusika moja kwa moja katika mashauriano ya ndani ya wiki kadhaa kati ya wafanyakazi wa vyeo vya juu wa Biden na spika McCarthy.

Forum

XS
SM
MD
LG