Marufuku hiyo ilikuwa inaendelea kutekelezwa Ijumaa ingawa Rais Buhari amesema Wanigeria wanaweza kuanza kutumia jukwaa hilo kwa ajili ya biashara na mawasiliano chanya.
Katika hotuba ya kuadhimisha siku ya uhuru wa Nigeria kiongozi huyo alisema kwamba kamati ya ofisi ya rais imeanza kuwasiliana na wakuu wa Twitter juu ya masuala kadhaa kuanzia usalama wa kitaifa na ulipaji kodi unaostahiki na namna ya kutanzua ugomvi. Twitter haijajibu bado kuhusu matamshi ya rais.
Serikali ya Nigeria ilisitisha shughuli za Twitter mwezi Juni baada ya kampuni hiyo ya mitandao ya kijamii kufuta ujumbe wa rais Buhari.
Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari