Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:20

BRICS: Mgawanyiko waripotiwa kabla ya mazungumzo ya upanuzi wa muungano huo


Viongozi na wawakilishi wa nchi wanacahama wa Brics
Viongozi na wawakilishi wa nchi wanacahama wa Brics

Viongozi wa muungano wa BRICS walikutana siku ya Jumanne kujadili mipango ya baadaye ya umoja huo wa mataifa yanayoendelea, lakini migawanyiko iliibuka tena kabla ya mjadala muhimu, kuhusu uwezekano wa upanuzi wa kundi hilo unaonuiwa kuongeza nguvu zake duniani.

Kuongezeka kwa mvutano kufuatia vita vya Ukraine na kuongezeka kwa ushindani wa Beijing na Marekani, kumesukuma China na Russia kuongeza juhudi za kutaka kuuimarisha muungano huo.

Wanachama wanataka kutumia mkutano wa kilele wa Agosti 22 hadi 24 mjini Johannesburg kuuongezea nguvu muungano huo, ambao pia unajumuisha Afrika Kusini, Brazil na India, ili kukabiliana na utawala wa Magharibi wa taasisi za kimataifa.

"Hivi sasa, mabadiliko duniani, katika nyakati zetu, na katika historia yanajitokeza kwa namna ambayo haijawahi kutokea hapo awali, na kuleta jamii ya wanadamu katika hali mbaya," Rais wa China Xi Jinping alisema katika hotuba yake aliyoitoa kwenye kongamano la biashara la BRICS.

Xi hakuhudhuria hafla hiyo, licha ya uwepo wa wenzake Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi. Rais Putin anashiriki mkutano huo kwa njia ya mtandao.

Forum

XS
SM
MD
LG