Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:44

Boti yapinduka Italia na kuuwa waliokuwa wakisheherekea siku ya kuzaliwa



Shughuli za uokoaji zikiendelea, baada ya boti iliyokuwa imebeba watalii kuzama katika ziwa Maggiore nchini Italia, Mei 28. Picha na VIGILI DEL FUOCO / AFP.
Shughuli za uokoaji zikiendelea, baada ya boti iliyokuwa imebeba watalii kuzama katika ziwa Maggiore nchini Italia, Mei 28. Picha na VIGILI DEL FUOCO / AFP.

Takriban watu wanne wamefariki dunia na mtu mmoja hajulikani alipo, baada ya mashua ya kitalii yenye urefu wa mita 16 kupinduka na kuzama kwenye Ziwa Maggiore kaskazini mwa Italia Jumapili jioni.

Wapiga mbizi wakisaidiwa na helikopta waliendelea kumtafuta mtu aliyepotea.

Ndege ya kubeba wagonjwa, magari kadhaa ya dharura, na ya zima moto, pamoja na Walinzi wa Pwani na polisi walihusika katika uokoaji na msako huo.

Huduma ya Taifa ya Zimamoto na Uokoaji ilisema watu 20 waliweza kuogelea hadi ufukweni au kuokolewa na boti nyingine, na watano kati yao walipelekwa katika hospitali za eneo hilo kwa matibabu.

Hata hivyo Juhudi za uokoaji zilizorota kutokana na mvua kubwa na giza, mamlaka zilisema.

Vyombo vya habari vya Italia viliripoti kuwa boti hiyo ilikuwa imebeba watu 25 wakiwemo abiria na wafanyakazi. Abiria walikuwa wakisherehekea siku ya kuzaliwa wakati dhoruba kali iliyozuka ghafla ziwani na upepo mkali kuipindua mashua hiyo

Taarifa ambazo hazijathibitishwa zilizopo katika vyombo vya habari vya eneo zilisema kuwa abiria hao walikuwa raia wa Uingereza, Italia na Israel.

Ziwa Maggiore ni kivutio maarufu cha watalii, upande wa kusini wa mlima wa Alps ulioko kwenye mpaka kati ya Italia na Uswizi.

Forum

XS
SM
MD
LG