Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 13, 2024 Local time: 09:33

Blinken aanza mazungumzo ya kikanda Riyadh kuhusu msaada wa kibinadamu Gaza


Waziri wa Mambo ya Nje ahudhuria mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Riyadh, Saudi Arabia, April 29, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje ahudhuria mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Riyadh, Saudi Arabia, April 29, 2024.

Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken amewasili Riyadh kwa ajili ya mazungumzo ya kikanda Jumatatu na Jumanne kuhusu msaada wa kibinadamu huko Gaza, mpango baada ya vita kwa maeneo ya Palestina, na utulivu na usalama katika Mashariki ya Kati.

“Waziri atajadili juhudi zinazoendelea ili kufanikisha sitisho la mapigano huko Gaza ambalo litasaidia kuachiliwa kwa mateka na jinsi Hamas ilivyo kati ya watu wa Palestina na sitisho la mapigano,” wizara ya Mambo ya Nje imesema.

Blinken atashiriki katika mazungumzo ya ngazi ya mawaziri wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba, ushirika wa wa kikanda wa nchi za Kiarabu zinazopakana na Ghuba ya Uajemi ambao unafanyaika katika mji mkuu wa Saudi Arabia.

Msemaji wa White House wa usalama wa taifa John Kirby alikiambia kituo cha televisheni cha ABC katika kipindi cha “This Week” leo Jumapili kwamba Marekani inaendelea kusukuma sitisho la wiki sita katika vita vya takriban miezi saba huko Gaza kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas.

Maungumzo ya sitisho la mapigano yamekuwa yakiendelea kwa miezi kadhaa, na licha ya vipindi kadhaa kuashiria kuwa makubaliano yalikaribia kufikiwa, Kirby hakutoa ishara ya maendeleo mapya katika majadiliano.

Amesema Israel imewahakikishia maafisa wa Marekani kuwa haitapeleka wanajeshi wa ardhini kusini mwa Gaza katika mji wa Rafah bila ya kusikiliza kikamilifu wasi wasi wa Marekani kwamba shambulizi kama hilo huenda likahatarisha maisha ya Wapalestina zaidi ya milioni 1 ambao wanapatiwa hifadhi huko.

Kirby amesema kwamba gati ya muda katika bahari ya Mediterranean inajengwa katika ufukwa wa Gaza na huenda ikakamilika katika muda wa wiki mbili au tatu ili iweze kusafirisha misaada zaidi ya kibinadamu katika eneo jembamba ili kuwasaidia Wapalestina walikumbwa na njaa.

Gaza, mpango wa baada ya vita

Mzozo wa kibinadamu huko Gaza ni mkubwa sana, licha ya ongezeko la misaada kila siku na Israel kuanza kutumia kivuko cha kaskazini na bandari ya Ashdod kwa ugawaji misaada wa kibinadamu.

Marekani inashirikiana na washirika kuweka njia ya majini kwa ajili ya kibiandamu; hata hivyo, juhudi hizi hazitoshi wakati idadi yote ya watu huko Gaza wanakabiliwa na hatari ya njaa na utapiamlo.

Maafisa wa Marekani wameelezea kwamba Washington ina nia ya dhati kusukuma upatikanaji wa amani ya kudumu na usalama kwa wote Waisrael na Wapalestina, ikiwa ni kupitia hatua thabiti ambazo zinaelnda kuwepo kwa taifa la Palestina ambalo litakuwa likiwa sambamba na la Israel.

Barbara Leaf, waziri mdogo wa mambo ya nje kwa masuala ya Near Eastern, amesema katika maelezo ya karibuni, “Ukingo wa Magharibi na Gaza lazima zunganishwe chini ya Mamlaka ya Palestina. Mamlaka ya Palestina ambayo ni muhimu kwa kuleta matokeo kwa watu wa Palestina kote Ukingo wa Magharibi na Gaza na kuweka hali ya utulivu”.

Washington pia imeeleza bayana kwamba Hamas isiwe na jukumu katika utawala.

Wachambuzi, hata hivyo, wanasema kuna vikwazo vingi kwa mtizamo wa Marekani.

Michael Hanna, mkurugenzi wa mipango katika International Crisis Group, ameelezea kwamba serikali ya sasa ya Israel imeonyesha “kukataa kabisa wazo la suluhisho la mataifa mawili.” Vile vile, “ukweli hali imebadilika sana tangu mwaka 1967 ambapo inafanya uwezekano wa kuwepo kwa taifa la Palestina kuwa jambo lisilowezekana.”

Ameiambia VOA, “hakuna uhakikisho wa kweli” kwamba nchi katika Mashariki ya Kati zina nia ya dhati kwa ujenzi wa baada ya vita huko Ukanda wa Gaza.

“Ni vigumu sana kwa pande hizi nyingi za kikanda kujihusisha kisiasa kwa wakati huu wakati vita vinaendelea.”

Matarajio kwa Saudi Arabia na Israel

Utawala wa Biden unaendelea kufanya kazi kwa upatikanaji wa makubaliano ambayo yatapelekea kuwepo kwa uhusiano wa kawaida na Israel, hata wakati baadhi ya maafisa na wachambuzi wanaona uwezekano huo ni mdogo sana.

Waziri Mkuu wa Israe Benjamin Netanyahu amepinga suluhisho la mataifa mawili na kurejea kwa Mamlaka ya Palestina kuidhibiti Gaza, matakwa ambao kwa kiasi kikubwa yanaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

Saudi Arabia imetaka, kama sharti, kuona nia ya dhati ya Israel kwa suluhisho la mataifa mawili.

“Kama misimamo ya Netanyahu haitabadilika, kwa hakika hataweza kuwa na uhusiano na Saudi Arabia. Huenda hilo ombi la Marekani na Saudi Arabia kwa uhsuiano kama huo limewekwa hadharani, kwahiyo Waisrael watakwenda kupiga kura, wanaweza kulichukua hili kama mbadala,” Nimrod Goren, mtaalamu wa masuala ya Israel katika Taasisi ya Mashariki ya Kati ameiambia VOA kwa njia ya barua pepe.

Marekani inatathmini shutuma za ukiukaji wa haki za vikosi vya IDF

Mikutano iliyopangwa ya Blinken huko Mashariki ya Kati inakuja wakati Marekani inatathmini habari mpya kutoka serikali ya Israel kuangalia iwapo baadhi ya vikosi vya jeshi la Israel viweke katika orodha ya ‘blacklist’.

Vikosi hivi vinashutumiwa kukiuka haki za binadamu za raia wa Palestina huko Ukingo wa Magharibi kabla ya mashambulizi ya kigaidi ya Oktoba 7 ya Hamas kwa Israel.

Forum

XS
SM
MD
LG