Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:45

Biden akusanya fedha zaidi kuliko Trump mwezi Septemba


Rais Donald Trump (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden
Rais Donald Trump (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden

Rais Donald Trump alikuwa amepitwa katika michango na mpinzani wake Mdemokrat Joe Biden mwezi Septemba ambaye anamshinda kifedha wakati zimebakia wiki chache kufikia siku ya uchaguzi.

Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa kampeni ya Trump, pamoja na Kamati ya Taifa ya Republikan, imekusanya dola milioni 247.8 mwezi Septemba, pungufu ya dola milioni 383 zilizochangishwa na Biden na Kamati ya Taifa ya Demokrat katika kipindi hicho hicho.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampeni ya Trump, Tim Murtaugh alituma ujumbe wa Twitter kuwa juhudi za Trump kukusanya fedha zilimwezesha kupata dola milioni 251.4 hadi mwisho wa mwezi Septemba, ikilinganishwa na dola milioni 432 zilizokusanywa na Biden.

Upungufu wa fedha kwa Trump wakati fulani ulikuwa haufikiriwi – kwa marais walioko madarakani katika uchaguzi kwa kawaida wanawapita kwa michango mahasimu wao – na inakuwa ni changamoto juu ya uwezekano wa kuchaguliwa kwake tena.

Kampeni ya rais ilikuwa inatarajia kuwa na fedha za kutosha katika akaunti ya benki ili kurusha kwa wingi matangazo ya Trump hewani na mitandaoni.

Lakini wiki iliyopita alipitwa katika kurusha matangazo na Biden kwa zaidi ya dola milioni 10, kwa mujibu wa kampuni ya kufuatilia matangazo ya Kantar/CMAG.

“Rais Trump anafikia kipindi cha mwisho cha kampeni akiwa na nguvu, rasilmali, rekodi na mbinu kubwa katika uwanja wa siasa kusambaza ujumbe na kushawishi kuchaguliwa tena,” Murtaugh ameeleza katika ujumbe wa Twitter.

Uchangishaji fedha wa Biden ulinufaika kutokana na kuongezeka hamasa ya wafadhili baada ya kifo cha Jaji wa Mahakama ya Juu Ruth Bader Ginsburg na kushuka kwa maoni jinsi Trump alivyofanya katika mdahalo wa kwanza wa rais.

XS
SM
MD
LG