Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:15

'Al-Shabaab' washambulia kituo cha polisi, mnara Kenya


Mnara wa mawasiliano ulioshambuliwa na al-Shabaab
Mnara wa mawasiliano ulioshambuliwa na al-Shabaab

Watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa ni wa kikundi cha kigaidi cha al-Shabaab wameshambulia kituo cha polisi cha Ijara kaunti ya Garissa  na pia kuharibu mnara wa mawasiliano nchini Kenya.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Kenya, kambi ya polisi iliyoko karibu na kituo cha polisi kilichoshambuliwa, iliweza kujibu mashambulizi hayo na kuwatimua waliofanya mashambulizi hayo, walipojaribu kukishambulia.

Eneo la Ijara linapakana na msitu wa boni ambao unadaiwa kutumiwa na kundi la al-Shabaab.

Wakazi wa eneo hilo wamedai kuwa washambuliaji hao wa al-Shabaab waliokuwa katika magari aina ya Landcruiser walihusika pia na wizi wa kwenye maduka katika kituo kikubwa cha biashara eneo la Ijara.

Kwa muda sasa serikali ya Kenya imeanzisha operesheni maalumu inayojulikana kama "operations Linda boni" dhidi ya al-Shabaab ambao wamekuwa wakijificha katika msitu mzito wa Linda boni ili kuwatokomeza.

Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa Mohammoud Saleh amethibitisha kwamba gari aina ya Landcruiser lililokuwa limeibiwa na al-Shabaab mapema leo limeonekana katika msitu wa Boni.

Pia amesema kuwa magaidi hao walihusika na kuharibu mnara wa mawasiliano wa shirika la simu la Safaricom.

Imelezwa na mkuu huyo kwamba wapiganaji hao wa al-Shabaab walifanikiwa kupora dukani na kutoweka bidhaa muhimu kama vile sukari, mafuta ya kupikia, maziwa, unga pamoja na vitu vingine baada ya kushambulia kituo cha polisi na kuiba gari.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Hubbah Abdi, Kenya

XS
SM
MD
LG