Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 11:35

Aliyekuwa mgombe urais Misri kufikishwa mahakamani


Aliyekuwa mgombea urais wa Misri Ahmed al-Tantawi akifanya mahojiano katika ofisi yake iliyoko Cairo Oktoba 12, 2023. Picha na Ahmed HASAN / AFP.
Aliyekuwa mgombea urais wa Misri Ahmed al-Tantawi akifanya mahojiano katika ofisi yake iliyoko Cairo Oktoba 12, 2023. Picha na Ahmed HASAN / AFP.

Mgombea urais wa zamani wa Misri Ahmed al-Tantawi atakabiliwa na kesi kwa kusambaza fomu za kuidhinisha uchaguzi ujao wa Misri bila idhini, mwanachama wa kampeni na watetezi wa haki alisema Jumanne.

Tantawi, ambaye aliondoa nia yake ya kugombea urais mwezi uliopita baada ya kushindwa kupata waungaji mkono wa kutosha ili kugombea, atakabiliwa na mahakama ya jinai kwa tuhuma za "kusambaza karatasi zinazohusiana na uchaguzi bila idhini rasmi", mtetezi mkuu wa haki za binadamu Hossam Bahgat aliandika kwenye mtandao wa X, zamani ukijulikana kama Twitter.

Mjumbe wa zamani wa kampeni yake alithibitisha kesi hiyo kwa shirika la habari la AFP, akisema "mawakili wao walishangaa kuona jina lake na la meneja wa kampeni" wakiwa miongoni mwa washtakiwa katika kesi hiyo.

Mbunge huyo wa zamani aliacha azma yake ya kugombea urais mwezi uliopita baada ya kudai kwa miezi kadhaa kwamba mamlaka za Misri zimekuwa zikimnyanyasa yeye na kampeni yake.

Hatimaye aliweza kukusanya ridhaa 14,000 tu kati ya 25,000 zinazohitajika ili kugombea, lakini aling’ang’ania kuwa angeweza kushinda dhidi ya rais aliyekuwa madarakani Abdel Fattah al-Sisi katika uchaguzi huru.

Katika kujaribu kuthibitisha kwamba anaungwa mkono na watu wengi, Tantawi alikuwa ametoa wito kwa wafuasi wake mwezi uliopita kuchapisha nakala za fomu ya kuidhinisha na kuzikabidhi kwa kampeni badala ya fomu rasmi zilizotolewa na halmashauri ya kusimamia uchaguzi. Orodha hiyo inamjumuisha Tantawi, meneja wake wa kampeni Mohamed Aboul Deyar na wajumbe wengine 21 wa zamani wa wakampeni ambao kwa sasa wako kizuizini. Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG