Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:56

Ajali ya basi yaua zaidi ya watu 32 nchini Misri


Picha ya baadhi ya magari yaliochomeka kwenye ajali ya Misri.
Picha ya baadhi ya magari yaliochomeka kwenye ajali ya Misri.

Basi moja la abiria limegonga gari lililokuwa limeegeshwa barabarani wakati kukiwa na ukungu mwingi mapema Jumamosi kwenye barabara kuu inayounganisha mji mkuu wa Misri, Cairo na ule uliyopo karibu na bahari ya Mediterranean wa Alexandria, na kuuwa tarkriban watu 32, kulingana na ripoti za mamlaka.

Ajali hiyo iliyohusisha magari mengine pia, ilipelekea baadhi kushika moto, na zaidi ya watu 63 kuachwa na majeraha, kulingana na wizara ya afya. Magari ya dharura yalifika eneo la ajali hiyo mara moja, huku yakianza kupeleka waliojeruhiwa hospitalini, wakati vyombo vya habari vikiripoti kuwa basi lililohusika lilikuwa likielekea Cairo kabla ya ajali hiyo kutokea.

Kwenye video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii, magari kadhaa yaliochomeka yanaonekana kando ya barabara, wakati wazima moto wakijaribu kudhibiti hali. Gazeti la kila siku linalomilikiwa na seriali la al-Ahram limeripoti kuwa magari 29 yamehusika kwenye ajali hiyo, iliyotokea kwenye mji wa Nubariya, takriban kilomita 160 kaskazini mwa Cairo.

Idara ya kitaifa ya hali ya hewa ya Misri siku moja iliyopita ilikuwa imeonya kuhusu ukungu mwingi kwenye baadhi ya barabara kuu. Ajali baya za barabarani huuwa maelfu ya watu kila mwaka nchini Misri kutokana na ubovu wa mifumo yake ya usafiri.

Nyingi ya ajali zinazotokea husababishwa na mwengo kasi, barabara bovu, pamoja na kutozingatia sheria za barabarani.

Forum

XS
SM
MD
LG