Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:22

Ajali ya moto Russia yaua watu wasiopungua 30 wakiwemo watoto watatu


Mlipuko uliosababisha moto katika kituo cha mafuta.
Mlipuko uliosababisha moto katika kituo cha mafuta.

Ajali ya moto kwenye  kituo cha mafuta katika mkoa wa kusini mwa Russia wa Dagestan Jumatatu jioni uliuwa watu wasiopungua 30 wakiwemo watoto watatu, wizara ya huduma za dharura ya Russia ilisema Jumanne.

Moto huo ulianza katika karakana ya kutengeneza magari pembeni ya barabara katika barabara kuu huko mji mkuu wa Dagestani wa Makhachkala Jumatatu usiku na kusababisha milipuko kadhaa huku moto ukisambaa kufikia kituo cha mafuta kilichokuwa karibu, maafisa walisema.

Picha zilizosambazwa na wizara ya huduma za dharura zilionyesha wafanyakazi wa zimamoto wakijaribu kuuzima moto mkubwa huku ukipanda juu angani wakati wa usiku.

Kanda za video zilizobandikwa kwenye mitandao zilionyesha jengo la ghorofa moja likiwaka, televisheni ya Reuters iliripoti.

“Wakati wa operesheni ya uokoaji huo huko Makhachkala, miili ya waathirika watatu zaidi iligundulika,” wizara hiyo ilisema kupitia ujumbe wa Telegram.

Kulingana na taarifa ya karibuni, kutokana na moto huo katika kituo cha mafuta watu 105 walijeruhiwa, na kati yao, 30 walifariki.

Kumi na tatu waliojeruhiwa walikuwa watoto, shirika la Interfax liliripoti mapema, likiinukuu wizara ya afya ya Dagestani.

Iliwachukua wafanyakazi wa zimamoto zaidi ya saa 3-1/2 kuuzima moto huo ulioenea katika eneo la mita za mraba 600, TASS iliripoti, ikikariri taarifa kutoka huduma ya dharura ya Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG