Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:49

Afrika Mashariki yaweka mikakati kukamilisha ujenzi wa reli ya SGR.


Kijana akipita karibu na reali iliyoko Kampala. Picha na LUIS TATO / AFP
Kijana akipita karibu na reali iliyoko Kampala. Picha na LUIS TATO / AFP

Kenya, Uganda, Rwanda, DRC na Sudan Kusini zimeamua kuweka nguvu ya pamoja kufanikisha ujenzi wa reli ya mwendo kasi SGR inayopita Afrika Mashariki.

Mawaziri wa uchukuzi kutoka mataifa hayo wamekubaliana kwa pamoja kutafuta wafadhili na wajenzi wa reli hiyo, kurekebisha mkataba wa maelewano na kuhusisha mataifa ya DRC na Sudan Kusini na vile vile jinsi ya kugawana majukumu ya kulinda reli hiyo ya SGR.

Waziri wa uchukuzi nchini Uganda Fred Byamukama amesema wamechukua mkondo huu kupunguza gharama ya kufanya biashara kuimarisha uchukuzi na kuunganisha mataifa hayo na pia kupunguza uchafuzi wa mazingira.

Uganda imefikia hatua za mwisho za mkataba kati ya wafadhili kufanya ujenzi wa SGR kutoka Mpakani Malaba hadi mji mkuu Kampala.

Naye waziri wa Uchukuzi wa Kenya Kipchumba Murkomen amebainisha kwamba Kenya itarejea katika ujenzi wareli ya SGR kutoka Naivasha kwenda mpakani Malaba mwaka huu kwa kima cha dola bilioni 5.3 ambazo inakusudia kupata kutoka sekta ya kibinafsi.

Ujenzi wa SGR Afrika Mashariki umegawanywa kwa vipande, kutoka Naivasha mpaka Malaba kisha Uganda itaunganisha Malaba na Kampala, sehemu ya tatu ni kati ya Kampala , Bihanga Kasese - Mpondwe mpaka DR Congo sehemu ya nne ikiwa kati ya Bihanga mpaka Milima ya Mirama na kisha mji mkuu Kigali Rwanda, sehemu ya tano ni kati ya Tororo – Gulu, mpaka Sudan Kusini Pakwach na Vurra.

Rwanda inapojiunga na msukumo huu waziri wa uchukuzi Jimmy Gasore amesisitiza umuhimu wa ushirikiano ambao utaharakisha na kupunguza mzigo wa kujenga reli ya SGR na hivyo kuwa ya faida kwa mataifa hayo .

Katika mkutano huo pia waziri Murkomen na mwenzake wa Uganda Katumba Wamala waliidhinisha mkataba wa maelewano kati ya Kenya na Uganda kufadhili ujenzi wa SGR kati ya Naivasha Kisumu Malaba na pia Malaba hadi Kampala baada ya makubaliano mwaka 2023.

Mwaka 2014 mataifa ya Kenya Rwanda na Uganda yaliweka makubaliano kujenga reli ya SGR kutoka Mombasa , Kampala mpaka Kigali Rwanda lakini ujenzi huo alisimamishwa ghafla mfadhili mkuu China ilipokukataa kuendelea kuufadhili baada ya kukosa maelewano na Uganda.

Forum

XS
SM
MD
LG