Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:00

Afrika Kusini yaifufua kesi ya mauaji ya wanaharakati dhidi ya utawala wa kibaguzi


Wanafunzi waliokuwa wakiandamana kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi katika Chuo kikuu Witwatersrand wakikimbia baada ya polisi kurusha mabobu ya kutoa machozi. Picha na Reuters/Ulli Michel
Wanafunzi waliokuwa wakiandamana kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi katika Chuo kikuu Witwatersrand wakikimbia baada ya polisi kurusha mabobu ya kutoa machozi. Picha na Reuters/Ulli Michel

Wizara ya sheria ya Afrika Kusini imesema siku ya Ijumaa kuwa inafungua tena uchunguzi kwa mauaji ya wanaharakati wanne wapinga ubaguzi, moja ya kosa mbaya sana ya uhalifu, lakini halijatatuliwa kwa takriban miongo minne.

Wanaharakati hao wanne waliokuwa wakiitwa Cradock Four walitekwa na kuuawa wakati walipokuwa wakijerea nyumbani eneo la Kusini mwa mji wa Cradock mwezi Juni 1985 baada ya mkutano.

Miili ya wanaharakati hao wanne-- Matthew Goniwe, Sparrow Mkonto, Fort Calata na Sicelo Mhlauli—iligundulika baada ya siku kadhaa, ikiwa imeungua vibaya na ikiwa na majeraha ya kuchomwa visu.

Vikosi vya usalama chini ya utawala wa kibaguzi vinashukiwa kuhusika na mauaji hayo. Lakini hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua za kisheria.

Waziri wa sheria Ronald Lamola amesema katika taarifa ya Ijumaa kuwa ilikuwa “ ni haki maslahi ya haki kwa familia za marehemu ambazo zimekuwa zikisubiri kwa miongo minne kujua ukweli kuhusuana na wahusika wa mauaji ya wapendwa wao “

Uchunguzi umefanyika mara mbili—mwaka 1987 na 1993—lakini uchunguzi huo ulizua maswali zaidi kuliko majibu”

Chanzo cha habari ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG