Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 27, 2025 Local time: 20:03

Afrika Kusini yaishitaki Israel kwa tuhuma za Mauaji ya Kimbari Gaza


Moshi ukifuka angani huko Kusini mwa Ukanda wa Gaza wakati wa mashambulizi ya Israel.Januari 3,2024. Picha na AFP
Moshi ukifuka angani huko Kusini mwa Ukanda wa Gaza wakati wa mashambulizi ya Israel.Januari 3,2024. Picha na AFP

Afrika Kusini imeishtaki Israel katika mahakama ya Umoja wa Mataifa kwa tuhuma kwamba kampeni ya kijeshi ya Israel huko Gaza sawa na mauaji ya kimbari.

Kuwasilisha kesi hiyo na uamuzi wa Israeli kujitetea katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki itaanzisha mapamabano au hali ya juu mbele ya jopo la majaji katika Great Hall of Justice.

Huenda kesi hii itachukua miaka mingi. Ni sehemu muhimu ya makubaliano ya kimataifa ya mwaka 1948 ya kuzuia na kuadhibu makosa ya jinai ya mauaji ya kimbari, ikiwa ni baada ya Vita vya Pili vya Dunia na Holocaust.

Mkataba huo wa kimataifa unafafanua kuwa mauaji ya kimbari ni kama vitendo vya mauaji “yaliyotendwa kwa azma ya kuharibu, lote au sehemu ya taifa, kabila, rangi au kundi la kidini.”

Maelezo ya kesi yaliyowasilishwa na Afrika Kusini yenye kurasa 84 yanasema vitendo vya Israel “vinasifa ya mauaji ya kimbari kwa sababu yana azma ya kufanya uharibifu mkubwa” kwa Wapalestina huko Gaza.

Imeiomba Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ ambayo pia inajulikana kama mahakama ya dunia, kutoa mlolongo wa hukumu kwa mujibu wa sheria.

Imeitaka mahakama kuitangaza Israel kuwa “imevunja na inaendelea kukiuka majukumu yake chini ya mkataka wa mauaji ya kimbari” na kuiamuru Israel kusitisha uhasama huko Gaza ambao unaweza kufananishwa na uvunjaji wa mkataba huo, kutoa fidia, na kulipia ujenzi kwa uharibifu uiioufanya huko Gaza.

Serikali ya Israel haraka ilikanusha madai ya mauaji ya kimbali. Taarifa ya Wizara ya mambo ya nje imesema kesi ya Afrika Kusini haina misingi ya kisheria na “haina maana na ukosefu wa heshina” kwa mahakama.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AP

Forum

XS
SM
MD
LG