Uhaba kwa kiasi unalaumiwa kwa ongezeko la mahitaji ukichanganya na kuvurugika kwa usambazaji, na biashara za haramu katika maeneo yenye mzozo.
Maafisa kadhaa katika mataifa ya Afrika ya kati wamesema wamiliki wa magari, madereva wa malori na pikipiki katika miji mikubwa wamekuwa wakisubiri kwa saa kadhaa, wakati mwingine siku kadhaa kujaza matanki yao, na imekuwa kawaida kwa vituo vya mafuta kuishiwa na mafuta mara kwa mara tangu uhaba wa mafuta ulipoanza miezi kadhaa iliyopita.
Maafisa wa Cameroon kwa kiasi fulani wamelaumu usumbufu unaoendelea unatokana na hali ya hewa ya dhoruba katika pwani ya Atlantiki, kukwamisha meli za mizigo katika bandari bandari iliyopo Lome, Togo ambayo ni kitovu cha kikanda.
Matatizo makubwa ya mafuta pia yamesababisha ghasia huko Chad. Maafisa wameripoti maandamano katika mji kuu N'djamena, na miji mingine ikiwemo ya Bongor, Moundou, Faya-Largeau na Abeche ambako jeshi wiki hii limewatawanya waandamanaji kwa kutumia gesi ya kutoa machozi .
Jeshi la serikali ya Chad limesema wiki hii kuwa wanajeshi wake wamekamata mamia ya makontena ya mafuta yaliyokuwa yakisafirishwa kwa magendo kwenda kwenye mpaka wa nchi hiyo na Sudan.
Forum